25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

BLAIR ATANGAZA KUREJEA KATIKA SIASA ZA UINGEREZA

LONDON, UINGEREZA


WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ametangaza kuwa anarejea tena kwenye siasa za Uingereza ili kupambana dhidi ya uamuzi wa kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya, maarufu Brexit.

Blair ambaye alikiongoza Chama cha Labour kuanzia mwaka 1994 hadi 2007, hata hivyo hatagombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 8.

Lakini ataunda vuguvugu la kisiasa juu ya majadiliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Blair (63), ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa muongo mmoja kuanzia mwaka 1997, alisema anafahamu uamuzi wake huu utakumbwa na ukosoaji mkali.

Lakini alisema si sawa kwake kuachia suala la Brexit liende kama liendavyo, bila kutoa mchango wake. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,207FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles