25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

TRUMP AMWALIKA DUTERTE IKULU MAREKANI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Philippines, Rodrigo Duterte, amepewa mwaliko kwenda Ikulu ya Marekani baada ya kufanya mawasiliano kwa simu na Rais Donald Trump.

Viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu vita yenye utata dhidi ya mihadarati inayoendeshwa na Duterte, ambayo imesababisha watu 7,000 kuuawa katika kipindi cha miezi 12.

Aidha wawili hao walijadili mzozo kuhusu Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa White House, Trump alifurahia mazungumzo hayo, na alitoa mwaliko huo, ingawa tarehe ya ziara hiyo bado haijapangwa.

Taarifa ya White House ilisema kuwa ziara hiyo itakuwa fursa ya kujadiliana kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa Marekani na Philippines, ambao kwa sasa unaendelea kuimarika.

Mwaka jana mkutano kati ya Duterte na mtangulizi wa Trump, Rais Barack Obama, ulifutiliwa.

Hatua hiyo ilifikiwai baada ya Duterte kumwita Obama ‘mwana wa kahaba.’

Awali Obama alimkosoa Duterte kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika vita yake dhidi ya wauza mihadarati.

Duterte ambaye kama Trump, alichaguliwa kuwa rais mwaka jana, amekuwa akisema anafurahia kuua mamilioni ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Trump mwenyewe ni mtu ambaye amekuwa akitoa matamshi ya kutatanisha.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,227FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles