26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

ETIHAD YATEUA MKURUGENZI MPYA

ABU DHABI, UAE


SHIRIKA la Anga la Etihad (EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group lenye jukumu la kuboresha utendaji na huduma zake duniani.

Halliday ataliongoza shirika hilo kuendana na huduma bora duniani na kuwasogeza karibu wateja kuendelea kufurahia huduma zinazotolewa na shirika hilo na washirika wake wa ndege.

Pia atawajibika kuwa karibu na wabia wa EAG na kushiriki vikao vya utawala vilivyo muhimu kwa mipango na maendeleo ya ukuaji wa biashara baina ya Abu Dhab na nchi za Falme za Kiarabu (UAE).

Halliday anajiunga EAG baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa wa miaka  30 katika Shirika la Ndege la Etihad na Kundi la Mashirika ya Kimataifa ya Ndege (IAG). 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,926FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles