NEW YORK, MAREKANI
HATIMAYE msanii wa muziki wa pop nchini Marekani, Madonna Ciccone, ameshindwa kesi ya kumzuia Darlene Lutz kutouza barua za kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Tupac Shakur.
Madona na Tupac walikuwa na uhusiano wa siri, lakini barua za Tupac ambazo zilikuwa zinaelezea uhusiano wake na mrembo huyo zilikuwa zinashikiliwa na Darlene Lutz na alitangaza kuziweka sokoni tangu mwaka jana, hivyo Madona alifungua mashtaka lakini inaonekana ameshindwa, hivyo barua hizo zinatarajiwa kupigwa mnada.
Moja ya barua hizo ni ile ambayo ilivunja uhusiano wa wawili hao mwaka 1995, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya Tupac kupoteza maisha mwaka 1996.
Barua hiyo iliandikwa maneno ya hisia kali, kulikuwa na ujumbe kama vile, kuwa na uhusiano na mtu mweusi kutamsaidia katika kazi yake na kwamba sura yake itaharibika iwapo ataanza uhusiano na mtu mweupe, ambaye ni Madona.