ATEMBEA NA JENEZA LA KAKA YAKE KISA KAM-MISS

0
590

MWANAUME aliyedai kum-miss kaka yake aliyefariki dunia mwaka jana, amefukua jeneza lenye mwili wake na kutembea nalo katika baiskeli mitaani, imeripotiwa juzi.

Mwanaume huyo, Elderlandes Rosa (29) aliwaambia polisi kuwa aliota kwamba kaka yake huyo Eri Erisberto, ambaye alifariki karibu mwaka mmoja sasa akiwa na umri wa miaka 30 alimtaka atekeleze ahadi yake ya kumtoa matembezini kwa baiskeli kama walivyokuwa wakifanya wakati akiwa hai.

Hivyo, akaenda katika makaburi ya mji na kulifukua jeneza lenye mwili wake huo, ambalo aliliweka nyuma ya baiskeli yake. 

Wakazi wa mji huo wa Prata, uliopo kusini mashariki mwa Brazil walitoa tarifa polisi baada ya kuhisi harufu kali ikitokea katika jeneza hilo wakati Rosa akitembea nalo mitaani usiku wa Jumapili iliyopita. 

Rosa awali alikataa kutii amri ya polisi waliojaribu kumsimamisha, na ambao walipanga kumkamata na kumtia pingu, kwa mujibu wa ripoti.

Baadaye aliripotiwa akiwaambia maofisa hao kuwa alilifukua kwa sababu alimkuwa amemkosa sana na kwamaba kabla ya kutemnbea naye akiwa jenezani mitaani alimtoa kutoka humo ili kuzungumza naye.

Afisa wa Polisi Luciano Goncalves alisema: 'Tulipokea simu kutoka kwa wakazi na tukaenda kuchunguza.

“Mwanaume huyu alisema kwamba ‘anamemiss’ sana kaka yake. Hivyo, alienda kufukua jeneza, akavunja mfuniko na kumtoa kuzungumza naye.' 

Amekamatwa kwa uhalifu wa kuighasi maiti, shitaka ambalo kiwango cha juu cha adhabu ni miaka mitatu jela na aliachiwa kwa dhamana akisubiri usikilizaji wa kesi yake.

Kufuatia tukio hilo la kushangaza vyombo vya habari vilimtafuta ili kumhoji. Rosa aliiambia televisheni ya Vitoriosa, kuwa kitendo chake hicho ni ahadi aliyomuahidi kaka yake wakati alipokuwa hai na hivyo ilikuwa lazima aitimize.

Anasema: 'Niliahidi kuwa iwapo yeye atatangulia kuaga dunia kabla yangu, ningemrudisha kumtembeza mitaani katika maeneo aliyopenda kutembelea wakati wa uhai wake. 

“Sasa nimetimiza ahadi hiyo na ninaendelea na kubakia mtulivu. Wale ambao wanataka kunicheka na kunifanya kikatuni, wanaweza kufanya wapendavyo. Mimi sijali ila mradi nimetimiza ahadi niliyoitoa. 

Hata hivyo, familia yake inasema kwamba ndugu yao huyo amekichukulia vibaya kifo cha kaka yake, tangu afariki dunia amekataa kukubali kama ameshaaga dunia.

Jeneza la kaka yake limesharejeshwa kaburini baada ya siku moja tangu lifukuliwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here