MUSEVENI AAMURU MABALOZI WA CHINA WACHUNGUZWE KWA UJANGILI

0
544

KAMPALA, UGANDA


RAIS Yoweri Museveni ameamuru kufanyika uchunguzi wa uwezekano wa maofisa wa ubalozi wa China kuratibu biashara ya nyara haramu nchini hapa.

Ujangili umekua kwa kasi katika miaka ya karibuni barani Afrika, ikichangiwa na ongezeko la mahitaji ya pembe za ndovu na faru barani Asia, ambako hutengenezewa dawa za kienyeji na sanamu.

Kwa mujibu wa Serikali, maofisa wa ubalozi wa China wanashukiwa kupanga misafara ya biashara hiyo ya pembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini, huku Uganda hutumika kama mapito makuu.

Msemaji wa Ofisi ya Mrakibu Mkuu wa Serikali (IGG), Ali Munira, hakuwataja wanadiplomasia hao wa China, lakini alisema Mamlaka ya Wanyama Pori Uganda (UWA) inachunguzwa.

Ubalozi wa China nchini hapa haukuweza kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo.

Museveni pia ameamuru uchunguzi mpya wa wizi wa pembe zenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja Novemba 2014.

Tayari maofisa watano wamesimamishwa UWA baada ya kutoweka kilo 1,335 za pembe kutoka ghala la mamlaka hiyo.

Matokeo ya uchunguzi wa awali hayakuwekwa hadharani, huku vyanzo vya habari vya polisi vilivyoshiriki vikisema inaonyesha Museveni hakufurahishwa na uchunguzi huo na intelijensia mpya inaonyesha uwezekano wa ushiriki wa maofisa wa China.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here