24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mhagama awataka wazazi, walezi kusimamia maadili kwa watoto

Na Maandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amewataka wazazi kutenga muda malezi kwa watoto ili kuwatizama na Kurekebisha mienendo yao.

Kauli hiyo ameitoa mapema Mei 5, 2024 aliposhiriki kama Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 69 ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini, sherehe zilizofanyika katika Kijiji cha Kilagano katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Waziri Mhagama amesema, mtoto anayelelewa kwa kuangalia mfano mzuri wa baba na mama lazima atakuwa na nidhamu na tabia njema.

“Wazazi tukae tutafakari utaratibu tunaotumia kulea watoto wetu ili wawe na madili bora katika katika Jamii,” amesema Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa jumuiya ya Wazazi mara baada ya kuhitimisha sherehe yao iliyofanyika katika Kijiji cha Kilagano halmashauri ya wilaya ya Songea.

Ameeleza kwamba lengo la kuanzishwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha inajenga maadili mema ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

Niendelee kuhimiza viongozi wa jumuiya ya wazazi ndani ya wilaya kwenye kata na kwenye matawi na kwenye Mashina tuendelee kulibeba jukumu hili.

“Kizazi kilichopo na hata kizazi kipya kimeathirika na maswala ya utandawazi na nguvu mpya ya Mawasiliano kama isipotumika vizuri itakuwa ni chanzo cha upotofu wa maadili,” amesema Waziri Mhagama na kuongeza kuwa:

“Tunahitaji wanachama wenye maadili, tunahitaji wananchi wa Peramiho wenye maadili,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Menace Komba ameishukuru Serikali na juhudi za Mbunge, Jenista Mhagama, walizofanya za kurekebisha mpaka wa Mlima Lihanje.

“Tulifanya mkutano na timu ya Mawaziri na tulifanya mkutano Kilagano na kuzungumza na wananchi na baadaye kufanikiwa kurekebisha mipaka ya Mlima Lihanje.

“Serikali ya wilaya itahakikisha  wananchi walioathirika na zoezi hilo kwa kuondolewa kwenye Mlima na kuwarudisha chini wanapata ardhi iliyotengwa kwa usawa,” amesema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akifurahia Jambo na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi katika sherehe yao iliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Kilagano Halmashauri ya wilaya ya Songea.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles