ARIANA GRANDE AMWEKEA ULINZI MKALI MAMA YAKE NEW YORK, MAREKANI

0
665

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Ariana Grande, ameweka ulinzi mkali kuzunguka nyumba ya mama yake, Joan kutokana na kuhofia usalama wake.

Wiki iliyopita msanii huyo alipokuwa Manchester Arena kwenye ziara yake ya muziki aliyoiita ‘The Dangerous Woman Tour’, dakika chache baada ya kumaliza shoo yake kulitokea mlipuko wa bomu na kusababisha watu 22 kupoteza maisha na wengine 119 kujeruhiwa.

Kutokana na hali hiyo, msanii huyo anaendelea kujilinda akihofia kwamba huenda mlipuko huo ulimlenga yeye na familia yake.

Kutokana na hofu hiyo, ameamua kumwongezea ulinzi mama yake kwa muda wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here