ANGELINA ATUMIA BIL 54 KUNUNUA NYUMBA MPYA

0
497

LOS ANGELES, MAREKANI


NYOTA wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie, ameonyesha jeuri ya fedha kwa kununua nyumba yenye thamani ya dola milioni 25 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 54 za Kitanzania.

Nyumba hiyo ya kisasa ipo maeneo ya Los Angeles nchini Marekani, huku ikitajwa kuwa miongoni mwa nyumba bora na zenye mvuto wa hali ya juu katika jiji hilo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 41, amefanya kufuru hiyo ikiwa ni miezi minane tangu kudaiwa kuachana na mume wake mwigizaji wa filamu, Brad Pitt.

Nyumba hiyo ina ukubwa wa mita za mraba 7,500, ipo maeneo ambayo wasanii wengi maarufu wanaishi akiwemo Casey Affleck, Natalie Portman, Lauren Graham, Will.I.Am na David Fincher.

Angelina na Brad walianzisha uhusiano wao tangu 2004 na mwaka 2014 walifunga ndoa, lakini wanadaiwa kuachana huku wakiwa na watoto sita ambao ni Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, Knox na Vivienne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here