26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hukumu kesi ya mtoto anayedaiwa kuvunjwa uti wa mgongo na mwalimu Februari 25

Elizabeth Kilindi – Njombe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Njombe, imesema hukumu ya kesi ya Hosea Manga, aliyekuwa mwanafunzi Shule ya Msingi Madeke, anayedaiwa kuvunjwa uti wa mgongo na mwalimu Focus Mbilinyi, inatarajiwa kutolewa Februari 25.

Februari 4 ilikuwa siku ya mahakama kupokea majumuisho ya ushahidi wa pande zote mbili ambapo majumuisho hayo yamewasilishwa mahakamani kwa njia ya maandishi.

Katika kesi hiyo, mashahidi upande wa Jamhuri walikuwa watano, huku upande wa mshtakiwa mashahidi wakiwa watatu akiwamo mshtakiwa mwenyewe. 

Kesi hiyo namba 141 ya mwaka 2019 ya Jamhuri dhidi ya Focus Mbilinyi imeendeshwa kwa takribani miezi minne.

Awali Hosea alieleza mahakama kuwa Machi 21, mwaka 2017 majira ya asubuhi, akiwa darasa la tatu Shule ya Msingi Madeke, mwalimu Mbilinyi alitoa zoezi la somo la Hisabati likiwa na maswali 10, huku akitoa maelekezo kuwa atakayekosa ataadhibiwa kwa idadi ya maswali aliyokosa.

Hosea alidai kuwa wakati mwalimu alipokuwa akiimiza ahadi yake kwa wanafunzi walioshindwa kufanya vizuri, yeye akiwa amekosa hesabu zote 10, ndipo akaambiwa atundike miguu juu ya dirisha, huku kichwa kikiwa chini na mwalimu kumwadhibu kwa viboko na baadaye akaangukia mgongo.

Mwalimu huyo naye wakati akijitetea, alidai Machi 21 mwaka 2017 ikiwa ni majukumu yake kazini alikwenda kufundisha darasa la tatu na mwisho wa kipindi akatoa zoezi la hisabati na baaadaye akiwa anasahisha ndipo akagundua wapo wanafunzi ambao walikuwa hawafanyi kazi alizokuwa anatoa darasani hapo akiwemo Hosea na wenzake.

Mwalimu alisema alichukua uamuzi wa kwenda kwa Mwalimu Mkuu Thomas Hongoli na kuomba ruhusa ya kutoa adhabu na akaruhusiwa kwenda kutoa adhabu ya viboko vitatu baada ya kufuata mchakato rasmi  wa utoaji wa adhabu ikiwemo kuandika kwenye kitabu cha adhabu na kuweka  kusaini.

Mwalimu Mbilinyi alidai kuwa baada ya kutoa adhabu ya viboko vitatu vya makalioni alitoka darasani na kuendelea na ratiba madarasa mengine na baadaye ndipo alipofuatwa na mwanafunzi  na kupewa taarifa kuwa Manga anaumwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles