25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Membe atinga Kamati ya Maadili CCM kuhojiwa

Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewasili Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 6, kwa ajili ya kuhojiwa na kamati ya maadili ya chama hicho.

Mbali na Membe, wengine wanaotakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ni makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Vigogo hao, walizua mjadala hivi karibuni baada ya zinzodaiwa kuwa sauti zao kusambaa mitandaoni wakizungumzia kupasuka kwa CCM.
Membe aliwasili asubuhi saa 3:10, akiwa katika gari lenye namba za usajili T 748 CNV Range Rover nyeusi.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alipokelewa na maafisa watano wa CCM ambao walimwongoza kuingia ndani ya ofisi.

Aidha, ulinzi katika viunga vya eneo hilo ‘White House’ umeimarishwa katika ofisi hizo ambapo kwa mara kwa kwanza Kampuni ya ulinzi ya Suma JKT ndiyo wanaolinda wakati siku za nyuma wamekuwa wakilinda raia wa kawaida huku waandishi wakizuiliwa kuingia getini.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles