Bujumbura, Burundi
SERIKALI ya Burundi imetangaza kuwa watu 700 wamefariki dunia kutokana na malaria nchini humo katika miezi miwili iliyopita.
Waziri wa Afya wa Burundi, Dk. Josiane Nijimbere amesema tangu mwanzoni mwa Januari hadi Machi 10 mwaka huu, watu zaidi ya milioni 1.8 wameambukizwa malaria.
Kwa mujibu wa Nijimbere, ugonjwa huo umeua watu 700 ambao ni wastani wa watu 10 kila siku.
Serikali ya Burundi imesema inahitaji dola za Marekani milioni 31 kukabiliana na maambukizi mapya ya malaria.
Mabadiliko ya tabianchi na umasikini wa kupindukia unaowakabili watu wengi nchini humo vimetajwa kuwa sababu ya vifo hivyo na mlipuko huo unaotokea wakati nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa.
Mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa kuna uwezekano malaria kutokomezwa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa na maradhi hayo kwa kiwango kikubwa, ifikapo mwaka