26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MALARIA YAUA WATU 700 NDANI YA MIEZI MIWILI

Bujumbura, Burundi


SERIKALI ya Burundi imetangaza kuwa watu 700 wamefariki dunia kutokana na   malaria nchini humo katika  miezi miwili iliyopita.

Waziri wa Afya wa Burundi, Dk. Josiane Nijimbere amesema tangu mwanzoni mwa Januari hadi Machi 10 mwaka huu,  watu zaidi ya milioni 1.8 wameambukizwa   malaria.

Kwa mujibu wa Nijimbere, ugonjwa huo umeua watu 700 ambao   ni   wastani wa watu 10 kila siku.

Serikali ya Burundi imesema inahitaji dola za Marekani milioni 31 kukabiliana na maambukizi mapya ya malaria.

Mabadiliko ya tabianchi na umasikini wa kupindukia unaowakabili watu wengi nchini humo  vimetajwa kuwa sababu ya vifo hivyo na mlipuko huo unaotokea wakati nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa.

Mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa  kuna uwezekano   malaria kutokomezwa  katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa   na maradhi hayo kwa kiwango kikubwa, ifikapo mwaka 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles