NEW YORK, MAREKANI
Rapa na mkali wa filamu nchini Marekani, Nick Cannon, anadaiwa kutoka na dansa Rozonda Thomas, baada ya kuachana na Mariah Carey.
Cannon na Rozonda, walionekana juzi wakipigana kisi jijini New York, hivyo kuwafanya mashabiki wa wawili hao wakiwa na maswali mengi.
Hata hivyo Rozonda kupitia akaunti yake ya Istagram, aliweka wazi kwamba wawili hao sasa wapo katika uhusiano na kila kitu kitazidi kuwekwa wazi siku hadi siku.
“Najua kuna maswali mengi yatakuwa yanaendelea, lakini huu ni ukweli kama inavyoonekana kwenye mitandao ya kijamii, kila kitu kitakuwa wazi siku hadi siku,” aliandika Rozonda