26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jela ilivyowapa kiki wapenzi wa mastaa hawa

Rihanna
Rihanna

NA BADI MCHOMOLO,

IMEKUWA kama mchezo vile kwa mastaa wa kiume wa Marekani kujivunia na kuona ustaa wao umekamilika pale ambapo watatia kwenye mikono ya Serikali na kwenda kuishi jela hata kama ni kwa muda mfupi.

Hali hiyo inachagizwa na ile hali ya kuona jela ni sehemu ya kukuza majina yao na muda mwingine kazi zao lakini wapo ambao dola za nchi zao zimewatia nguvuni kutokana na makosa na siyo kwa sababu wana kiu ya kukuza majina yao.

Zaidi Ujuavyo wiki hii limekuandalia orodha na nyota mbalimbali nchini humo ambao wapenzi wao walizidi kujizolea umaarufu walipokwenda jela.

Rihanna

Huyu ni msanii wa Pop nchini , kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Work’, ambao amemshirikisha rapa Drake, huku tetesi zikidokeza kwamba wawili hao ni wapenzi.

Awali mrembo huyo alikuwa anatoka na msanii wa RnB Chris Brown, uhusiano wa wawili hao ulianza tangu Chris alipotoa wimbo wake wa With You.

Wimbo huo ulidaiwa kumgusa sana mwana dada Rihanna na kushindwa kuficha hisia zake za mapenzi hivyo akajipeleka mwenyewe mikononi mwa Chri Brown na penzi lao likaanza rasmi.

Inadaiwa kwamba Chris ni msanii mwenye hasira za karibu na maera kadhaa wamekuwa wakigombana ila mwama 2013, Chris alikwenda jela mara baada ya kumshushia kichapo mrembo huyo.

Penzi lao likawa limefika mwisho na kuwashangaza mashabiki wao wengi ambao hawakuwahi kufikiri kama Chris na Rihanna wanaweza kuachana.

Akiwa jela, Chris Brown alizidi kuwa maarufu kutokana na kuanza kutoka kimapenzi na mwanamitindo Karruache Tran.

Hata pale alipotoka jela penzi lake likawa kwa mwanamitindo huyo na akamsahau kabisa Rihanna na wawili hao walitengeneza kapo yenye nguvu licha penzi hilo kutodumu.

Whitney Houston

Alikuwa mke wa rapa Bobby Brown, alipoteza maisha tangu mwaka 2012, wawili hawa walifanikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa ambaye naye alipoteza maisha mwezi juni mwaka jana.

Bobby kama kichwa cha familia alikuwa ndiyo chanzo cha migogoro katika nyumba yao kutokana na kuvunja sheria mbalimbali zilizopangwa.

Moja ya shida aliyokuwa nayo Bobby ni ile ya kunywa pombe kupita kiasi na kupelekea Januari 17 mwaka 2000 kutia nguvuni kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Kwa kosa hilo Bobby alikwenda jela kwa siku nana huku akitozwa faiani ya dola 2000 na yeye kutoka dola 800 na kufanya kazi mbalimbali za kijamii. Alipoma;lizia kufumikia kifungo hicho cha nje aliendelea kurudi jela kwa makosa mbalimbali.

Tameka

Huyu ni mke wa rapa Clifford Joseph Harris maarufu kwa jina la T.I, wawili hao wamefanikiwa kupata watoto watano, T.I amekuwa mtu wa matukio mengi nchini Marekani na inadaiwa kwamba ni miongoni mwa wasanii wa Hip hop ambao wanalisumbua jeshi la polisi mara kwa mara.

Mwaka 1998, mke wa T.I, Tameka alikuwa na wakati mgumu baada ya rapa huyo kukamatwa na polisi baada ya kukutwa na bangi, lakini baada ya kufikishwa mahakamani alihukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi za kijamii, lakini msanii huyo alionekana kuendelea kufanya makosa mengine.

Mwaka 2004, msanii huyo alikutwa na kosa lingine la uvunjaji wa sheria za nchi hivyo alitakiwa kwenda jela kwa miaka mitatu, Tameka alipambana kuhakikisha mume wake haingii tena jela, mfurulizo wa matukio yake yamezidi kumpa jina rapa huyu mtukukutu.

Shanell

Alikuwa ni mpenzi wa Lil Wayne, lakini wawili hao walikuja kuachana mwaka 2010 mara baada ya Lil Wayne kutoka jela. Lil Wayne aliingia jela kwa miezi nane kutokana na kumiliki silaha kinyume na sheria, lakini baada ya kutoka msanii huyo alizidi kuwa maarufu kwa kurekodi nyimbo kali.

Aisha Atkins

Huyu ni mke wa rapa Ja Rule, walifunga ndoa tangu mwaka 2001, mrembo huyo anadaiwa kuwa na moyo wa ujasiri baada ya mume wake kwenda jela kwa miaka miwili lakini alikuwa mvumilivu na kumsubiri rapa huyo.

Baada ya Ja Rule, kutoka jela aliamini kuwa hawezi kuwa na mrembo huyo, lakini alipokelewa na kuendelea na uhusiano wao. Rapa huyo alikwenda jela kwa kosa la kufanya matukio ya uharibu kwa kutumia silaha.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles