Huddah ajutia kupoteza usichana wake

Huddah Monroe
Huddah Monroe
Huddah Monroe

NAIROBI, KENYA

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, ambaye jina lake halikauki kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, Huddah Monroe, amedai kwamba anajisikia aibu kuharibu usichana wake huku akiwa bado anaishi na mama yake.

Mrembo huyo ameweka wazi kwamba alivunja usichana huku bado akiishi na mama yake, hivyo anadai kuwa amemkosea mama yake.

“Kila nikikumbuka naumia sana, maana sikuwa na lengo la kupoteza usichana wangu mapema tena nikiwa nyumbani kwa mama yangu, baada ya kugundua kwamba nimetoa bikira yangu nilikuwa nashindwa kumuangalia mama.

“Kila wakati nilihisi kwamba amejua nini nimekifanya, hivyo nilikuwa na aibu sana kwa mama yangu, lakini ndivyo hivyo ilivyotokea. Najua mama alinisamehe kwa hilo kwa kuwa nilimuomba radhi,”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here