Imechapishwa: Tue, Nov 14th, 2017

LULU DIVA: SINA MPINZANI

Na ESTHER GEORGE


MSANII anayekuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, amesema hana mpinzani katika kazi zake na anaamini juhudi zake zitamfikisha alipokusudia.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lulu Diva, alisema anaamini atafika mbali kimuziki kutokana na kuwekeza akili zake katika kazi zake.

“Napenda kile ninachokifanya, naamini nitafika mbali hivyo naona sina mpinzani kwani hakuna wa kunizuia kufika nilipokusudia, namwamini Mungu na nitafika levo za kimataifa,” alisema.

Lulu Diva alisema anapambana kuhakikisha anatoa nyimbo nzuri ambazo zina ujumbe kwa jamii na matumaini yake ni kuufikisha muziki wake nje ya nchi.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

LULU DIVA: SINA MPINZANI