27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BENZEMA: RONALDO NI MBINAFSI KULIKO MIMI

MADRID, Hispani


MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema, amesema anaamini Cristiano Ronaldo ni mbinafsi zaidi yake, lakini ni kwa faida ya Real Madrid na hana tatizo na mchezaji huyo bora duniani.

Mfaransa huyo amecheza na Ronaldo kwa takribani muongo mmoja, baada ya wawili hao kujiunga na mabingwa wa La Liga kabla ya msimu wa 2009-2010.

Benzema amepata mafaniki tele katika kipindi alichokuwa Hispania, ingawa anaamini mafanikio yake kwa kiasi fulani yamefichwa na Ronaldo. Hata hivyo, haoni tatizo na hilo na alisema kuwa yeye na Mreno huyo wana uhusiano mzuri.

“Nafunga mabao, lakini mtu mwingine akifunga mabao  50 kwa msimu huwezi kufanya kitu. Ni tofauti na nilivyocheza Lyon. Napenda soka na kushinda mataji. Nafurahia sana.

“Ronaldo na mimi tunaelewana vizuri. Napenda kucheza naye. Anapenda kugongeana mpira. Ni mbinafsi kuliko mimi, lakini hiyo ni kawaida. Hili halinisumbui. Mwisho wa yote ni vizuri kwa ajili ya timu,” alisema Benzema.

Akizungumzia alivyoweza kudumu muda mrefu Madrid, Benzema alisema hilo limemshangaza kwa kiasi fulani ingawa anaamini amepitia matatizo mengi kwani  vyombo vya habari vinapenda kuuza habari kwa kupitia yeye. Hata hivyo, mchezaji huyo alisema hatishwi na matukio yoyote na amejizatiti katika mchezo.

“Sikuwahi kudhani kama ningedumu miaka tisa Madrid. Nilipokuwa Lyon, nilikuwa nikiwaza kwenda Real Madrid kushinda mataji. Jambo gumu zaidi Madrid ni presha.

“Gumzo kuhusu mimi? Ni wauza magazeti tu. Nimezoea. Nimeelekeza akili yangu kwenye soka, nimejifunza kukaa kimya,” alisema Benzema.

Benzema pia alimzungumzia kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ambaye aliwahi kuinoa Real Madrid mwaka 2010 hadi 2013, akimsifia kwa kumsaidia kuwa mchezaji bora.

“Mourinho alinisaidia sana. Ni tabia yake kuwezesha wachezaji.Ni kocha mzuri,” alisema.

Benzema ambaye amefunga mara moja katika mechi saba za Ligi Kuu Hispania msimu huu, atarejea Real Madrid Novemba 18 dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles