23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

HATIMA YA JUX, VANESSA FIESTA DAR

Na KYALAA SEHEYE


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Vanessa Mdee, amesema hatima ya kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Juma Mpolopoto ‘Jux’, iko mikononi mwa mashabiki wa Jiji la Dar es Salaam katika tamasha la Tigo Fiesta, litakalofanyika Novemba 25 mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club.

Vanessa amesema hayo baada ya kumpa kazi ya kumwimbia katika tamasha la Fiesta lililofanyika mkoani Morogoro, ili amshawishi kurudiana naye, lakini Jux alishindwa na kumwambia itabidi awaulize mashabiki wa Dar es Salaam watakaoamua warudiane ama la.

“Leo umeshindwa kabisa kuimba wimbo wa kunishawishi mimi kurudiana na wewe, sasa kilichobaki ni Novemba 25 katika Jiji la Dar, mashabiki wataamua kama mimi kuendelea kuwa na wewe ama la,” alisikika Vanessa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles