VIGOGO wa Serie A, AC Milan, watamkosa Zlatan Ibrahimovic katika mchezo wa kesho dhidi ya Liverpool, ambao ni wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ibrahimovic anaendelea kuuguza majeraha, hivyo taarifa kutoka Italia zimedai hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachokwenda England kwa ajili ya mtanange huo utakaochezwa Anfield.
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza goti, mkongwe huyo alirejea dimbani wikiendi iliyopita dhidi ya Lazio, ambapo alifunga katika ushindi wa mabao 2-0.
Mbali ya huyo, pia imeelezwa kuwa kiungo wa Milan, Sandro Tonali, alikosa mazoezi ya asubuhi ya leo, hivyo huenda naye akashindwa kuikabili Liverpool.