30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kocha afungashiwa virago Serie A

IKIWA ni mechi nne tu zimechezwa msimu huu, Verona ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) imemfukuza kazi kocha wake, Eusebio Di Francesco.

Di Francesco (52), amefukuzwa baada ya Verona kufungwa bao 1-0 na Bologna, matokeo yanayoiacha ikiwa mkiani mwa msimamo.

“Hellas Verona FC inatangaza kusitisha majukumu ya Eusebio Di Fransesco kama mkuu wa benchi la ufundi,” imesomeka taarifa ya Verona.

Kocha huyo aliajiriwa majira ya kiangazi, mwaka huu, kuchukua nafasi ya Ivan Juric aliyetimkia Torino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles