24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

ZITTO ATUA DODOMA, KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI LEO

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anashikiliwa na polisi mkoani Dodoma wakati akisubiri kukabidhiwa kwa  Kamati ya Bunge Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kwa mahojiano.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimola amethibitisha kushikiliwa kwa mbunge huyo ambapo amesema wamemuhifadhi ‘pahala’.

“Tumempokea saa tatu asubuhi hii na tumemhifadhi pahala hadi saa nane mchana tutakapomkabidhi kwa Kamati ya Maadili itakapokutana,” amesema Kamanda Kimola.

Zitto alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam jana akitokea Kigoma na kusafirishwa kuelekea Dodoma leo saa 10 alfajiri leo.

Kukamatwa kwa mbunge huyo kunatokana na agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyeagiza kamati hiyo ya Bunge kumhoji kwa kauli yake kuhusu kamati na ripoti za tanzanite na almasi kuwasilishwa serikalini badala ya bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles