23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WIZKID: CHRIS BROWN ANANIBEBA

Chris Brown na Wizkid

 

 

LAGOS, NIGERIA

BAADA ya wimbo mpya wa Ayodeji Balogun (Wizkid) ujulikanao kwa jina la ‘Afrikan Bad Gyal’ kufanya vizuri kwenye vyombo mbalimbali vya habari, msanii huyo ameweka wazi kuwa anabebwa vizuri na mkali wa RnB nchini Marekani, Chris Brown.

Wimbo huo, ambao umeachiwa wiki iliyopita, huku akimshirikisha msanii huyo, unaonekana kufanya vizuri kwa kipindi kifupi ndani na nje ya Nigeria, hivyo anaamini ushirikiano wa Chris unazidi kumfanya awe juu.

“Afrikan Bad Gyal ni wimbo ambao unaweza kupigwa sehemu yoyote, ninashukuru kuona unafanya vizuri, Chris Brown amezidi kuupa nguvu wimbo huo, japokuwa si mara ya kwanza kufanya naye kazi, lakini safari hii ameonekana kunipa nguvu zaidi, nawashukuru sana mashabiki wangu kwa sapoti wanayonipa,” alieleza Wizkid.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles