23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Kilimo yaweka kambi Monduli kupambana na nzige

Na Upendo Mosha, Monduli

Wizara ya Kilimo imeweka kambi katika eneo la kata ya Engaruka Wilayani Monduli, mkoani Arusha, kudhibiti na kuangamiza makundi mapya mawili ya nzige yalivamia eneo hilo yakitokea nchi jirani ya Kenya.

Helkopita mbili za shirika la kupambana na nzige wekundu kutoka nchini Zambia na Ethiopia zimewasili na kuanza kazi ya kupulizia sumu katika eneo hilo, baada ya kumaliza kuangamiza nzige katika maeneo ya wilaya ya Mwanga,Siha, Simanjiro na Longido.

Akizungumza na Waandihi wa Habari, Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda, wakati akipokea Helkopta za Shirika hilo, katika kata ya Engaruka wilayani Monduli,alisema ujio wa helkopta hizo kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuwaangamiza nzige.

Alisema nzige walioingia katika eneo hilo ni kundi jipya ambapo katika muda wa siku mbili wataangamizwa na kwamba kazi kubwa iliyobaki ni kushughulika na nzige hao mpakani mwa Kenya na kuhakikisha hawaingi tena nchini.

“Kama tumemaliza maeneo yote ya awali ambapo nzige hawa walipoingia …kazi iliyobaki hapa ni ndogo kutokana na kwamba tayari ndege moja imekuja na zipo nyingine mbili zitaingia hapa kwa hiyo leo na kesho tutawaangamiza na katika eneo la kiteto ambalo tulidhani wataingia mpaka sasa hatujapa taarifa za uwepo wa nzige,”alisema.

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda, alisema nzige hao mpaka sasa hawajaleta madhara yeyote wa binadamu Wala mimea na kwamba simu inauotumika haijapigwa kwenye makazi ya watu ushambukia mimea na kwamba inayoendelea kupigwa.

“Mapambano yanaendelea vizuri sana na helkopta hizo zitqbaki hapa kwa miezi mitatu kuhakikisha hakuna nzige hata mmoja atakaye salia na pia natambua mchango wa wataalamu ambao wapo porini kupambana ni matumaini yetu kwamba kazi hii tutaimaliza bila tatizo…muhimu muongeze juhudi na mimi nitakuwa hapa,”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Iddy Kimanta, alisema baada ya kupata taarifa alihakikisha anashirikiana na viongozi wa vijiji pamoja na kata kupambana na kundi hilo.

“Baada ya taarifa ya uwepo wa kundi hilo jipya hili nilishirikiana na viongozi wa vijiji kukagua na kufuatilia mahala walipo kaa ili kazi ya kuwaangamiza iwe rahisi na tumefanikiwa naamini baada ya nguvu kuongeza na wizara tutalimaza,”alisema

Naye Mkuu wa wilaya ya Monduli, Edward Balele, alisema nzige hao walifamia katika eneo lenye ukubwa wa kati ya Hekta 45-50 na kwamba hawajaleta madhara yeyote zaidi ya kushambukia maeneo machache yamalisho.

February 19, Mwaka huu karibu Mkuu wa wizara hiyo Gerald Kusaya,alitoa taarifa rasmii ya uwepo wa kundi la nzige walioingia nchini na kutua katika wilaya za Mwanga na Siha mkoani Kilimanjaro

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles