28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana waliohitimu mafunzo ya SIDO Simiyu watakiwa kijiajiri

Na Derick Milton, Simiyu

Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo nchini (SIDO) Mkoa wa Simiyu, limetoa mafunzo kwa vijana 15 kutoka katika kaya zilizopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF III) mkoani humo ya jinsi ya kutengeneza nguo aina ya batiki pamoja na usindikaji wa vyakula.

Vijana hao kutoka Wilaya za Maswa, Bariadi, Busega na Itilima wamepatiwa mafunzo hayo kwa muda wa mwezi, huku wakitaka a kwenda kijiajiri wenyewe kwani mafunzo waliyopata yatawasaidia kujiletea maendeleo wao wenyewe na familia zao.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Festo Kiswaga, akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotenezwa na vij ana waliopata mafunzo ya ujaslimali kutoka SIDO(Picha na Derick Milton).

Akifunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo Cha Maendeleo ya jamii Bunhmala, mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, ametaka vijana hao kuhakikisha elimu ambayo wameipata inawaondoa katika umaskini wao wenyewe na familia zao na kuwa na familia zenye kipato.

“Mafunzo haya ambayo mmepata msiende uko na kuanza kutafuta kazi ili mkaajiliwe, nendeni mkajiajiri wenyewe, msipende kuajiriwa hamtapata maendeleo, nendeni mkajiajiri Elimu hii ambayo mmepata ni kubwa Sana, Elimu ya kuongeza thamani vyakula, kutengeneza nguo ndiyo ujaslimali wa sasa,” amesema Kiswaga.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka vijana kutumia changamoto zilizopo katika jamii zao kuwa fursa, huku akiwaleleza kuwa soko la mafunzo ya ujaslimali ambao wamepata ni kubwa Sana hivyo hawana budi kulitumia.

Aidha amelipomgeza Shirika hilo kwa Elimu ambayo wametoa, ambapo ameeleza mafunzo kulenga vijana ambao wanatoka kaya maskini ni ubunifu wa hali ya juu, na itazifanya kaya hizo kuondokana umaskini jumla na itasabanisha uwepo wa viwanda vingi vidogo.

Hata hivyo Kiswaga amewataka SIDO kufanya ufuatiliaji kwa vijana na kuwakagua mara kwa mara maendeleo yao, ili kuangalia malengo ambayo yalilengwa Kama yamefikiwa ikiwa pamoja na kuangalia mitaji ambayo wamepewa kama wameitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Awali akiongea katika hafla ya kuhitimu kwa vijana hao Meneja SIDO Mkoa, Atanasi Moshi, amesema kuwa mafunzo yametolewa kwa vijana kwa ushirikiano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo katika Mkoa wa Simiyu Vijana 18 ndiyo walitakiwa kupata mafunzo hayo.

Moshi amesema kuwa mbali na kuwapata mafunzo, vijana hao watapatiwa mtaji kiasi cha Sh 200,000 kwa kila mmoja, lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa wajaslimali na wanaweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo bila ya kuwa na kisingizio cha mtaji.

Amesema kuwa mafunzo ambayo wamepewa vijana hao yanahusu jinsi ya kutengeneza nguo aina ya batiki, vyakula vya kusindika ambapo wamefundishwa jinsi yakuongeza thamani kwenye vyakula ambavyo alisema vinawazunguka katika mazingira yao.

Meneja huyo ametaka vijana hao kwenda kutumia elimu na ujuzi walioupata kwa kujiletea maendeleo kwani walichofundishwa ni kikubwa sana na Kama watakitumia ipasavyo kitawafikisha kwenye malengo yao waliojiwekea na hawatakuwa maskini tena.

Naye, Salama Maduka, mmoja wa vijana waliohitimu mafunzo hayo, amesema kuwa elimu waliyoipata ni kubwa na inaenda kubadilisha maisha yao kwani mbai na elimu wamepatiwa na mtaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles