29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

TEC yatoa wito kwa viongozi wa Kanisa Katoliki

Na Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amesema Mapadri 25, Masista 60 na Wazee wawili wa Baraza la Walei wamefariki dunia ndani ya miezi miwili kwa sababu mbalimbali ikiwemo suala la upumuaji.

Padri Kitima ameeeleza hayo leo Jumatano Machi 3, 2021 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali hasa mlipuko wa ugonjwa wa corona katika Ofisi za Makao Makuu ya TEC Kurasini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, akizungumza na Waandihi wa Habari leo Machi 3, 2021 Dar es Salaam.

Padri Kitima amesema Viongozi Mapadri hao walifariki dunia ndani ya miezi miwili kuanzia Desemba Mwaka jana hadi Februari, mwaka huu.

Aidha, amewataka waumini kuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya ikwemo kusafisha mikono na maji tiririka.

“Zaidi ya Mapadri 25 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu wa kupumua, Masista zaidi ya 60, kwa miezi mitatu mfululizo wakati si kawaida, huwa wanapoteza maisha lakini si kwa wingi huu kwa hiyo ifike mahali tuambiane ukweli kuwa corona ipo na tunahitaji kuchukua tahadhari kwa hali ya juu kuhusiana na hili.

“Tupo kwa rezima na tupo tukisherekea uhuru wa mwanadamu kushikamana na Mungu, tukijiandaa kusherekea Pasaka Watanzania na waumini wanatakiwa kufata maelekezo ya Wizara ya Afya kimwili na viongozi wa dini kiroho,”amesema Padri Kitima.

Aidha, Padri Kitima, amesema Watanzania wanatakiwa kujua kwamba mtu anatakiwa kulinda uhai wake na wa mtu mwingine.

“Kila mmoja wetu wanatakiwa kujua jinsi ya kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Wizara ya afya ili kuepuka vifo kwa viongozi wa dini na waumini na Watanzania wote.

“Februari 24, Mwaka huu, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Dk. Dorothy Gwajima) aliweka na kuainisha tahadhari zinazotakiwa kufatwa ili kuepukana na ugonjwa huo, tutawasaidia kwa kuwapa ulinzi na msaada kwa kutokuwa chanzo cha maambukizi kwa kunawa, kuvaa barakoa.

“Sisi kama Viongozi wa dini Kanisa Katoliki tumeshuhudia vifo vya Mapadri wanaofanya kazi ya kuhudumia wangonjwa na wamepatwa na tatizo hili la kupumua, lakini changamoto tunayoipata ni kuwa hatuwezi kuthibitisha kama ni corona.

“Kwa kuwa sisi hatuelezwi na Madaktali na hao madaktari sio wote wanaruhusiwa kupima na kuthibitisha kwa kuwa wizara imeweka utaratibu wake, lakini kwa kuwa vifo vinatokea kotekote tunawaomba Watanzania wachukue tahadhari zaidi,” amesema Padri Kitima.

Amesema kila Mtanzania amehusika kwa namna moja au nyingine katika kushiriki msiba wa watu wanaokufa kwa tatizo la kupumua.

Pia amesema; “Nchi nyingi zinapima na kusaidia watu kupata idadi ya wagonjwa na kuwasaidia hali inayoendelea inatutaka kuwasikiliza sana viongozi wetu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

“Viongozi tunapenda kushirikiana katika kupigania uhai wa Watanzania kwa kila mtu kulinda uhai wake na uhai wa mtu mwingine kwa kupata taarifa za kiafya,” amesema Padri Kitima.

Aidha, ameongeza kuwa wanasayansi ni wakati wao wa kufanya uchunguzi kuhusiana na ugonjwa wa kupumua ili kuweza kupata taarifa kuhusu Watanzania.

“Ukweli unamuweka mtu huru, tuache kusema kuwa tukiwaambia ukweli watu tutakuwa na hofu hapana inatakiwa waambiwe ili wajue kuwa ni kitu cha kweli ugonjwa fulani unaua,” amesema Padri Kitima.

Pia amesema kuwa vifo vilikuwepo lakini sio kwa wingi wa kiasi hiki kinachoendelea kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hongera TEC kwa mara nyingine kusema ukweli bila ya kuficha
    Ila mimi sielewi mnaposema “amewataka waumini kuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya ikwemo kusafisha mikono na maji tiririka.”
    Tutakuwa tunarudia malimau. tangawizi na nyungu, vyote ambavyo havikusaidia kuondoa Corona
    Wizara na serikali inakataa kufuata ushauri wa wataalamu wa ndani na nje, hasa shirika la afya duniani (WHO), pamoja na chanjo.
    Tafadhali TEC zungumzeni na hili pia bila ya kutafuna maneno. Kama walivyofanya chama cha mawakili na wanasheria

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles