25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

EWURA yawataka wananchi kutojiunganishia umeme kinyemela

Na Shomari Binda, Musoma

Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wananchi kuepuka kuunganisha umeme majumbani kupitia mafundi wasiotambulika maarufu kama vishoka.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Ewura, George Mhina, wakati akizungumza kwenye kikao na viongozi watendaji wa Wilaya ya Musoma.

Amesema kuna hatari kubwa kuunganisha umeme majumbani kwa kuwatumia mafundi ambao hawajapewa lesenu kutoka Ewura.

Mhina amesema Ewura licha ya majukumu yake mengine ikiwemo kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wateja wanaopata huduma ya nishati na maji lakini pia wanahusika na utoaji wa leseni.

Amesema licha ya leseni za uanzishaji wa vituo vya mafuta lakuni wanatoa leseni kwa mafundi wanaounganisha umeme majumbani.

Kuna hatari kubwa kuwatumia mafundi wasiotambulika katika kuunganisha umeme majumbani ikiwemo kuunguliwa nyumba na kuunguza vifaa vingine vya umeme.

“Tupo Mkoa wa Mara na baadae tutaenda Geita katika kutoa elimu kwa umma juu ya masuala mbalimbali na kazi zinazofanywa na Ewura ikiwa ni pamoja na kupokea malalamiko,”amesema Mhina.

Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk.Vicent Naano, amesema Ewura inapaswa kufungua ofisi mikoani ili kuwasikiliza wananchi kwa karibu.

Amesema ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ambayo yanapaswa kusikilizwa na Ewura na kuwapatia wananchi ufumbuzi na sio kuwa na ofisi si ya Kanda pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles