30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Silaa aweka utaratibu mpya wa kazi kwa Maafisa wa sekta ya Ardhi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuanzia sasa watumishi wa sekta ya ardhi nchi nzima wanaohusika na Upangaji, Upimaji na Umilikishaji watafanya kazi siku mbili ofisini na siku tatu za wiki watafanya uwandani (Site).

Waziri Silaa amesema hayo Aprili 15, 2024 wakati akifanya uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi ya jijini Mbeya inayofanyika katika ukumbi wa Mkapa, Sokomatola mjini Mbeya.

Waziri Silaa amesema amefanya mawasiliano na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuweka utaratibu na kuwaandikia rasmi watumishi hao wa sekta ya ardhi katika ofisi za Halmashauri.

Amesema watumishi hao wa sekta ya ardhi nchi nzima watakuwa wanafanya kazi ofisini siku za jumatatu na ijumaa na siku za jumanne, jumatano na alhamisi watakuwa wanafanya kazi wakiwa uwandani tu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles