25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mufti Mkuu azungumzia miaka 60 ya Muungano

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Abubakar Zuberi, amezungumzia miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, huku akiwaalika viongozi na wauminin wote wa kiislamu waliopo mkoani Dodoma kushiriki katika Dua ya pamoja kuelekea maadhimisho ya Muungano itakayofanyika Aprili 22, 2024, Dodoma.

Pia amewapongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi kwa uzalendowa kutunza na kuzilinda tunu za Muungano kama zilivyoasisiswa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Shekh Abed Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 16,2024 jijini Dar es Salaam, amesema Baraza limepokea mualiko wa kushiriki Dua hiyo itakayofanyika Dodoma na kuongozwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwaalika viongozi na waumini wa dini ya kiislamu waliopo Dodoma na Wilaya zake na mikoa jirani kushiriki kwa wingi kwenye tukio hilo muhimu kwa Taifa ambapo mimi Mufti wa Tanzania nitashiriki pia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles