24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WAZIRI MKUU INDIA KUIPATIA UGANDA MASHINE YA SARATANI

KAMPALA, UGANDA


WAZIRI Mkuu wa India Narendra Modi amefanya ziara nchini hapa na kuahidi kuipatia Uganda mashine ya kisasa ya kutibu ugonjwa wa saratani.

Akitokea Rwanda alikosaini mikataba minane, Modi yu Uganda, ambako alikutana na jamii ya Wahindi kabla ya kulihutubia bunge la nchi hiyo baadaye jana.

Pia atashiriki mkutano wa kilele wa wafanyabiashara wa Uganda na India, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS.

Mara baada ya kuwasili mjini Entebbe, Modi alikutana na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni, ambapo wawili hao walifanya mazungumzo na kusaini mikataba kadhaa ya kibishara kama alivyofafanua Museveni.

“Kwa upande wetu tumesisitiza juu ya biashara, uwekezaji na utalii, kwa sababu haya ndiyo mambo matatu yanayoweza kuwaweka watu pamoja, ambako tunafanya kazi kwa ajili ya manufaa yetu sote. Tunapoweza kusaidia maendelea ya watu wa India kwa kununua bidhaa zao, na wanaweza kusaidia maendeleo yetu kwa kununua bidhaa zetu,” Museveni alisema.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Uganda, nchi hiyo iliagiza bidhaa za thamani ya dola milioni 774 kutoka India, huku nchi hiyo ikiiuzia India bidhaa zenye thamani ya dola milioni 38 tu.

Naye Modi alisema, “Kama ishara ya urafiki wetu kwa watu wa Uganda, Serikali ya India imeamua kutoa mashine ya kisasa ya matibabu ya saratani kwa taasisi ya saratani ya Kampala, alisema.

“Nina furaha kubainisha kuwa mashine hii si tu itatimiza mahitaji ya marafiki zetu wa Uganda, lakini pia mahitaji ya marafiki zetu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki.”

Uganda ina jamii kubwa ya  Wahindi, likiwemo kundi la wamiliki wa viwanda waliofanikiwa baada ya kurudi kudai mali zao walizopokonywa wakati wa utawala wa Rais Idi Amin.

Mwaka 1972, Amin aliamuru kufukuzwa kwa watu wa jamii ya Asia, wengi wao wakiwa Wahindi, kutoka nchi hiyo ya Afrika Mashariki, akisema alitakwa kuurejesha uchumi mikononi mwa wenyeji.

Sehemu kubwa ya mali walizonyanganywa zimerejeshwa kwa wamiliki wake wa awali chini ya utawala wa Rais Museveni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles