28.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

‘POLISI WANAONGOZA KWA RUSHWA IRINGA’

                                                                             |Raymond Minja, Iringa 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa imetoa taarifa ya utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu ambapo inaonyesha polisi wanaongoza kwa kutupiwa lawama za rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Aidan Ndomba amesema taaisisi hiyo imepokea malalamiko 142 katika kipindi cha  Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu kati ya malalamiko hayo malalamiko 42 yamefunguliwa majalada ya uchunguzi, malalamiko 100 yamefanyiwa uchunguzi wa awali na kutolewa ushauri kwa walalamikaji.

“Idara zinazoongoza kulalamikiwa kwa rushwa Mkoa wa Iringa ni Jeshi la polisi ambapo malalamiko 20 yalipokelewa, mabaraza ya ardhi malalamiko 14,watendaji wa serikali za mitaa (kata na vijiji) pamoja na Halmashauri za Wilaya.

“Jumla ya mashauri mapya 12 yamefunguliwa mahakamani katika kipindi hicho na kufanya jumla ya mashauri 21 kuendeshwa katika mahakama,” amesema Ndomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles