20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

MKANDA WA SAUTI, TRUMP AKILA NJAMA ZA KUFICHA TUHUMA KASHFA INAYOMKABLI WAVUJA

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump amesikika akijadili na mwanasheria wake binafsi namna, anavyoweza kununua haki ya simulizi kutoka nyota wa ngono, ambaye alidai kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Uwapo wa mkanda huo, ambao ulirekodiwa kwa siri na mwanasheria wake wa muda mrefu, Michael Cohen miezi miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu 2016, uliripotiwa wiki iliyopita na gazeti la New York Times, ambalo lilisema Shirika la Upelelezi Marekani (FBI) liliukamata wakati walipovamia ofisi za Cohen mwaka huu.

Unamhusisha Karen McDougal, mwanamitindo wa zamani wa utupu, ambaye alisema aliwahi kuwa na uhusiano wa miezi kadhaa na Trump baada ya kukutana mwaka 2006 muda mfupi baada ya mke wa Trump, Melania kuzaa mwanao Barron.

Katika mkanda huo, Trump na Cohen wanazungumzia ununuzi haki ya simulizi ya McDougal, ambayo aliiuza mwezi mmoja kabla kwa Jarida la National Enquirer kwa dola 150,000.  Jarida hilo kamwe halikuichapisha simulizi hiyo.

Wakati wa urekodi wa mkanda huo, Cohen anasikika akisema anataka kuanzisha kampuni itakayochukua haki za American Media, kampuni inayoimiliki Enquirer.

Wakati wa kampeni, timu ya Trump ilikana kufahamu mpango wa  mauziano baina ya McDougal na American Media.

Lakini katika mkanda huo, mgombea urais-Trump haonekani kushangazwa wakati suala hilo linapojitokeza wala hoja ya Cohen juu ya umuhimu wa kuirudishia kampuni hiyo kile ilichomlipa McDougal.

‘Nahitaji kuunda kampuni kwa kusafisha habari zote hizo kuhusiana rafikio yetu David,” Cohen anasema katika kile kilichoonekana kumaanisha David Pecker, bosi wa American Media.

“Wakati utakapofika muda wa kugharimia, kitu ambacho kitakuwa –,” Cohen anasema, kabla ya Trump kuingilia na kuuliza kugharimia nini?”

“Tunapaswa kulipa –,” Cohen anasema, kwa mujibu wa mkanda huo ilionao CNN, ambao pia ulihusisha mazungumzo mengine ya biashara baina ya wawili hao.

“Hatutolipa kwa fadha tasilimu?” Trump anasikika akiuliza katika kipande ambacho ni sehemu ngumu kuisikia vyema.

Cohen kisha anasikika akisema, hapana hapana, lakini kile kilichofuata pia hakikusikika.

Mkanda huo ulitengnezwa Septemba 2016, miezi miwili kabla ya Uchaguzi Mkuu na ulikabidhiwa CNN na mwanasheria wa Cohen, Lanny Davis.

Cohen, ambaye amefarakana na Trump, anachunguzwa na FBI kuhusu shughuli zake za biashara na iwapo malipo holele waliyofanya yalikiuka sheria za kampeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles