23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri Jaffo ampa maagizo mawili Kasesela

NA  FRANCIS  GODWIN,IRINGA

WAZIIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa  maagizo mawili kwa Mkuu  wa  Wilaya ya  Iringa, Richard Kasesela.

Miongoni mwa maagizo hayo, ni kuwakamata na kuwachukulia  hatua kali wananchi  wanaochafua mazingira na  kufikishia  agizo kwa Wakala  wa Wakala  wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kutengeneza  barabara  ya kwenda Shule ya  Sekondari  Kihesa.

Akizungumza  na wanafunzi na  walimu  wa Shule ya  Sekondari  Kihesa jana,    Waziri  Jafo  alisema shule hiyo imekuwa ya kwanza nchini kwa  kufanya  vizuri  katika ukusanyaji wa  chupa  za  plasitiki ambazo  zimekuwa  zikitupwa  ovyo  mitaani na wananchi  wasiojali mazingira .

Alisema kwa  kuweka  mkakati kabambe  wa  kuwawajibisha  watu wanaochafua  mazingira,  utasaidia  miji  kuwa katika hali ya  usafi.

Alisema  wajibu  wa  kutunza mazingira,  ni wa  kila mmoja na ndio maana  Rais Dk.  John Magufuli  alianzisha  usafi  kila  mwisho  wa  mwezi nchi  nzima.

“Lazima  kila  mmoja  wetu  kuunga  mkono jitihada  mbalimbali  zinazofanywa na rais wetu Dk.  John Magufuli katika  maendeleo…hata  suala  hili la usafi ni wajibu wetu  sote  kuweka mazingira katika hali ya usafi,asitokee  mwingine  anafanya usafi na  mwingi   anachafua,”  alisema  waziri Jafo

Alimtaka Kasesela   kufikisha salamu  zake kwa  Meneja  wa  TARURA  Mkoa  wa Iringa  kuhakikisha anatengeneza barabara ya kutoka Semtema hadi Kihesa  ili iweze  kupitika   wakati  wote  tofauti na  ilivyo sasa.

“Mkuu wa wilaya  nakuagiza   kawaambie  TARURA,waziri  nimeagiza  barabara  hii  ifanyiwe  ukarabati  hata kama  si kwa kiwango  cha lami,itengenezwe  kwa  kiwango  cha changarawe  na iweze  kupitika   vizuri “

Wakati  huo  huo,Waziri Jafo  aliwataka  wananchi kushiriki katika  uchaguzi  wa Serikali za Mitaa na vijiji  ambao unataraji kufanyika mapema  mwezi  ujao .

” Mwaka  2019,  ni   mwaka wa uchaguzi wa  Serikali za Mitaa, nawapongeza  Watanzania wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha  kwa mara  ya  kwanza  tumevunja  rekodi,  maana  lengo  letu  lilikuwa  tuandikishe watu  milioni 22.9  waliojiandikisha  ni  milioni 19.6 sawa na asilimia 86,”alisema.

MWISHO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles