25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Waliokata mkono wa albino, kukimbia nao jela maisha

*Ilikuwa wauze mganga wa kienyeji Sh mil 6

Na  Walter   Mguluchuma-Katavi.

WAKAZI wanne  Tarafa ya  Mamba Wilaya ya    Mlele  Mkoa wa  Katavi, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya  kukutwa na  hatia  ya kutaka kumuua  mtu mwenye ulemavu wa ngozi kwa kumkata mkono wake, kisha kuondoka nao  kwa lengo la kwenda kuuza kwa mganga wa kienyeji Sh milioni 6.

Waliohukumiwa kifungo hicho jana, ni Alex   Manyanza  Maliganya , Galila  Nkuba (Malago) na   Shile  Dalushi.

Hukumu hiyo, ilitolewa  na    Jaji   Richard  Mashauri wa Mahakama Kuu ya   Kanda ya  Sumbawanga  katika  Mahakama ya  Hakimu  Mkazi   ya   Mkoa wa   Katavi, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa  mahakamani    na upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi 12.

Upande wa mashtaka uliwakilishwa na wanasheria wawili wa Serikali, Simon    Peres na  Dickson Makoro na washtakiwa walitetewa na mawakili,Elis Kifunda na  Patrick Mwakyusa .

Awali katika kesi hiyo, wandesha  mashtaka na wanasheria wa Serikali walidai washtakiwa kwa pamoja walienda kosa hilo Mei 14,2015 katika   Kijiji cha Kinganda  saa 6 usiku .

Walidai siku ya tukio, watuhumiwa walikwenda nyumbani  kwao na  mtu  mwenye ulemavu wa  ngozi, Lime   Luchoma  ambaye  alikuwa amelala  chumbani.

Walipofika walipojaribu kumuua kwa kumkata  mkono wake wa kulia,kisha kuondoka  nao.

 Walidai baada ya kuchukua mkono mzima waliondoka nao, kisha kuubanika kwenye moto ili iwe rahisi kwao kuusafirisha kwenda kwa mganga wa kienyeji aliyekuwa amewaagiza.

Katika  utetezi  wao,washtakiwa waliiomba   mahakama  iwaachie huru kwa sababu maelezo waliyotoa mbele ya  mlinzi wa  amani katika Mahakama ya  Mwanzo ya  Mpanda Mjini walikiri kufanya kitendo hicho kutokana na kupata mateso ya kupigwa na polisi .

Wakili wa  washtakiwa wa kwanza na wa pili,    Eliasi Kifunda aliomba mahakama imwachie  huru  washtakiwa  kutokana na kuwa na familia kubwa inayomtegemea na tangu kipindi ambacho amekaa mahabusu miaka 4 sasa  familia yake imekosa  malezi .

Pia  mshtakiwa  huyo bado ni kijana  mwenye umri wa  (28),akipewa  nafasi ya kusamehewa  anaweza kujirekebisha .

Mshtakiwa wa pili, aliomba mahakama  iangalie    kutoa adhabu ambayo  inaweza kuwa na   nafuu kwake  kutokana na yeye kuwa na mri wa (44) familia yake inahitaji malezi yake .

Kwa  washtakiwa watatu na wanne,Galila Nkuba  na  Shile  Dalushi,  waliokuwa wakitetewa na wakili Patrick   Mwakyusa ambaye  kwa upande wa mshtakiwa watatu  aliomba  huruma ya jaji  kwa kuwa  mshtakiwa huyo  ana watoto tisa wanaomtegemea.

Mshtakiwa wa nne, aliomba  mahakama   imwachie huru kwa kuwa  ana  umri bado mdodo wa (31) na mkewe amefariki wakati akiwa mahabusu  na ameaacha watoto watatu  na kosa hilo ni la kwanza kwake .

Peres  aliiambia   Mahakama  baada ya utetezi huo, kuwa  matukio  ya ukataji wa  viuongo  vya watu wenye ulemavu  wa ngozi  ni  ukatili ambao hauvumiliki duniani.

Alisema hali hiyo, inawafanya watu  watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoishi  kwa amani  katika dunia hii waliopewa na Mungu.

Alisema wengi wao, wamelazimika kuwa wakimbizi  kwenye makazi ya  familia zao  na kuishi kwenye maeneo tengefu.

Akisoma  hukumu  hiyo, Jaji     Richald  Mashauri  aliiambia  Mahakama kutokana na ushahidi uliopelekwa  mahakamani na upande wa mashtaka pasipo   mashaka yoyote yale imeona washtakiwa wanayo hatia .

 Alisema ushahidi  uliouwa ukitolewa na upande wa   utetezi wakati wa kusikiliza kesi hiyo umekuwa   ukitofautiana, hali ambayo haiwezi  kuiifanya mahakama   kushawishika na kuwaona washtakiwa hawana hatia. Pia wazee washauri wa   Mahakama wote kwa pamoja  walisema kwenye maoni yao washtakiwa walitaka kuua .

Washtakiwa  wametiwa hatiani chini  ya kifungu  cha  sheria 211(a)  cha  sheria ya  adhabu  sura  namba 16   marekebisho ya mwaka 2002.

Katika kesi hiyo, mahakama  ilimwachia huru mshtakiwa wa sita,  Masunga  Kashindye ambaye   baada ya kuchiwa alitimua mbio na kuelekea kusikojulikana ambapo mshtakiwa wa tano, Maiko   Samweli  alifariki  dunia wakati akiwa mahabusu.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles