23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

RC aagiza ujenzi wa choo uwanja wa mpira

BEATRICE MOSSES, MANYARA

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexandre Mnyeti amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza ujenzi wa choo eneo la kiwanja cha mpira wa miguu kutokana na eneo hilo kuwa na watu wengi.

Mnyeti ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa halmashauri hiyo kwenye mkutano wa hadhara ambapo mmoja wa wananchi alitoa ombi hilo.

Mkazi wa Mbulu mjini, Robert Bayo amesema eneo hilo lina watu wengi na ni eneo ambalo watu wanafanya biashara zao lakini wakihitaji huduma ya choo inawabidi kwenda kuomba kwenye nyumba za watu.

“Katika hali fulani ya kusema tusiharibu mazingira watu wengine unakuta wanajipenyeza, sasa sisi tulikuwa tunataka kujua katika hali hii viongozi wa wilaya wana utaratibu gani kutuwekea choo kwenye eneo hili ambalo tunafanyia biashara?”, Alihoji Bayo.

Mnyeti naye akamuuliza mkurugenzi wana mpango gani wa kujenga choo kwani wanakusanya ushuru kwenye vibanda hivyo vya biashara.

Akijibu swali hilo Mkurugenzi huyo alisema tayari michoro imeshachorwa na wanatarajia kuanza ujenzi mwezi ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles