24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ataka wenye ulemavu kujishughulishi

Na Gaudency Msuya, Rufiji

SERIKALI imewataka watu wenye ulemavu nchini kuiga mfano wa wakulima wa mazao mbalimbali wa Wiliaya ya Rufiji ambao wamekuwa wakijihusisha na uzalishaji wa mazao bila kujali hali zao za ulemavu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhghulikia Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa, alitoa wito huo jana alipokuwa akifunga mafunzo ya usalama mahala pakazi kwa wakulima 150 wenye ulemavu wilayani Rufiji.

Alisema amefurahishwa na kitendo cha watu wenye ulemavu wilayani hapa kjihusisha na kazi za kilimo ambazo wengi wa walemavu wamekuwa wakikwepa kwa kisingizio hawawezi kufanya kazi ngumu kutokana na ulemavu wao wa viungo.

“Nimefurahishwa mno na wakulima hawa ndiyo maana nimetoa wito kwa wengine kuiga mfano huo kwa sababu mbali ya kuongeza kipato chao lakini pia kinasababisha wasiwe ombaomba,”alisema Ikupa.

Alisema Serikali itahakikisha inawaunga mkono walemavu hao ili waweze kuzalisha mazao ya chakula na biashara bila vikwazo hatimaye mbali ya kuongeza kipato cha ngazi ya familia lakini wataweza kchangia pato la oaifa.

Ofisa Mafunzo wa Taasisi inayojihusisha na Usimamizi wa Masuala ya Usalama Mahala pakazi (OSHA), Glory Biniventure, alisema wameamua kuwapa mafunzo hayo waklima wenye ulemavu ili waweze kufanya kazi zao bila khatarisha afya zao.

“Wakulima hawa wanahitaji kufanya kazi katika mazingira yaliyo salama na hawawezi kufanya hivyo bila kupewa mafunzo, ndiyo maana tumekuja kwao kuwajengea uelewa”alisema Glory.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) Wilaya ya Rufiji, Said Mussa, aliishkuru Serikali kwa kutambua umuhimu wa wenye ulemavu na kamua kuwapelekea mafnzo hayo ambayo alisema anaamini yatawajengea uelewa wa kutosha.

“Tunamshkuru waziri kwa kukubali kuja kwetu wenye ulemavu na pia tunampongeza Rais Johna Magufuli kwa kuwajali wenye ulemavu na tunamhakikishia kuwa nasi tuko bega kwa bega naye,”alisema Said.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles