23.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

Andengenya aonya wanasiasa wanaopandikiza chuki

Na Editha Karlo-Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, amewataka wanasiasa kuacha kutoa kauli za kuchonganisha wananchi na Serikali ili wawaunge mkono katika kampeni zao jambo ambalo ni kinyume na sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya nchi yetu.

Akizungumza na waandishi wa habari alisema hivi karibuni kumeibuka madai ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakidai Serikali ya mkoani Kigoma inawanyanyasa wananchi kwa kuwabambikiza kesi na kuwatishia kuwa wasichague vyama vya upinzani na wakifanya hivyo watanyang’anywa uraia.

“Hivi karibuni Mgombea Mwenza wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, alitoa kauli zinazosikika katika mitandao ya kijamii akieleza maswala ya uraia na unyanyasaji, huo ni upotoshaji wa makusudi na uchochezi,”alisema.

Alisema Mkoa wa Kigoma ni mkoa ambao wakimbizi na wahamiaji haramu wengi kutoka nchi jirani wamekuwa wakikimbilia, hivyo hufanya uwepo wa hamiaji wengi ambao si raia wa Tanzania.

Alisema Serikali inapotoa huduma kwa raia wake inawajibu wa kufahamu na kuwatambua raia wake, mbali na masuala ya ulinzi na usalama ni lazima ijiridhishe kuwa rasilimali zinazotolewa zinawafikia wananchi wake hivyo lazima ijiridhishe.

“Mkoa wa Kigoma haujawahi kunyanyasa raia au mtu yeyote asiye raia kwa kigezo cha kuwa yeye amechagua upinzani, ikumbukwe Mkoa wa Kigoma una wakimbizi zaidi ya 32,000 tangu waingie mwaka 1972 na wanaishi katika vijiji 73 vilivyopo hapa na hawajawahi kubaguliwa wala kunyanyaswa kwasababu Serikali inawatambua,” alisema.

Andengenye alisema hakuna ukweli wowote wa hayo matamko wanayo toa baadhi ya viongozi wanaogombea wananchi wote wanahudumiwa kwa usawa amewataka wanasiasa hao kuacha kueneza uongo kwa lengo la kutaka kupigiwa kura au kuungwa mkono.

Alisema vyombo vya dola vyote hudusani idara ya uhamiaji vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na hawajawahi kufanya jambo lolote kinyume na sheria au kinyume na haki za binaadamu na kuwanyima watu haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles