26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mgombea urais NCCR aahidi neema Mara

NA SHOMARI BINDA, MUSOMA

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha NCCR Mageuzi, Jeremia Makanja, amewaahidi wananchi wa Mkoa wa Mara kunufaika na rasilimali zilizopo kwenye mkoa huo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye eneo la stendi ya Nyasho Manispaa ya Musoma, alisema wananchi wa Mkoa wa Mara hawapaswi kuishi katika mazingira magumu.

Alisema Mkoa wa Mara kutokana na takwimu zilizopo ni miongoni mwa mikoa ambayo inazalisha dhahabu kwa wingi lakini wananchi wake hawanufauki na rasilimali hiyo.

Bakanja alisema iwapo atapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atahakikisha  rasilimali za Mkoa wa Mara zinawanufaisha pamoja na taifa kwa ujumla.

Alisema licha ya dhahabu, utalii ni eneo ambalo linaweza kuupa uchumi mkubwa Mkoa wa Mara iwapo utasimamiwa vizuri na kuomba kuchaguliwa ili awape neema wananchi.

” Nyie wananchi wa Mkoa wa Mara mnazo fursa nyingi ambazo mnaweza kunufaika nazo iwapo kutakuwa na usimamizi mzuri.

” Hapa lipo Ziwa Victoria na upo uwezejano was kufanya utalii wa ziwani na ukainua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla kanichagueni Oktoba 28 ili tuweke mambo vizuri”, alisema Makanja.

Alisema licha ya Mkoa wa Mara amezunguka katika maeneo mengine ya Tanzania na kuona rasilimali ambazo bado hazijatumiqa vizuri na kuwaletea manufaa wananchi.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma mjini kupitia chama hicho, Joyce Sokombi, alisema akichaguliwa kwenye nafasi hiyo atashirikuana kwa karibu na mgombea urais ili kusukuma maendeleo ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles