25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Kunenga aonya watakaofanya fujo siku ya uchaguzi Oktoba 28

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyofanya fujo siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jana jijini Dar es Salaam, Kunenge alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama.

Alitoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kutumia haki yao ya msingi na kutijokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura.

“Hii itawasaidia kuchagua viongozi wanaowataka wao kwa maendeleo yao ya sasa nayabaadae kwao na vizazi vyao.

“Hali ya amani na utulivu kwenye jiji letu la Dar es Salaam ni shwari na itaendelea kuwa shwari siku zote hivyo hakuna sababu ya wananchi kuwa na wasiwasi.

“Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika October 28 ambapo Rais Dk. John Magufuli amepanga iwe siku ya mapumziko ili kila mwananchi aweze kupata nafasi ya kupiga kura,”alisema Kunenge.

“Nitumie fursa hii kutoa onyo kwa kikundi chochote cha watu au mwananchi yoyote, kama anataka kufanya fujo ndoto hizo azifute kwa kuwa tumejipanga kisawa sawa.

“Nilipata nafasi ya kuhudhuria kampeni na niweona wagombea wanatoa sera nzuri kiasi kwamba wananchi wanatakiwa kujitokeza kuwapa nafasi waweze kutekeleza walichowaahidi,”alisema Kunenge.

Alisema wakazi wa Dae es Salaam ni vyema wakajitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuweza kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi.

Katika hatua nyingine, jana alitembelea Bandari ya Dar es Salaam, kuangalia makontena yenye vifaa vya mradi wa stendi ya kisasa Mbezi Louis.

Akizungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo Kunenge, alisema amekuta agizo la kuachiwa makontena hayo ili kuweza kumalizia stendi hiyo ambayo agizo lake halijatekelezwa jambo linalopelekea miradi hiyo kushindwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa na kuleta kero kwa wananchi.

Pamoja na hayo Kunenge alisema kutoka kwa haraka kwa ujenzi wa Stand ya Mbezi Louis itasababisha kazi kufanyika kwa haraka na itakuwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli alilotoa wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi na kuagiza mradi ukamilike kabla ya mwishoni wa Novemba.

Pia Kunenge alitoa siku mbili makontena 13 yenye vifaa vya ujenzi wa Stand ya Mbezi yaliyokuwa yamekwama bandarini yaanze kutoka baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara na Mamlaka ya Mapato TRA.

Sanjari na hayo ametoa wito kwa taasisi za Serikali zinazohusika kufanikisha miradi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles