29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

WAVULANA WAONGOZA KUZOA SIFURI KIDATO CHA SITA

Na MWANDISHI WETU


BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita uliofanyika Mei 2018, ambao wavulana wameongezeka kupata sifuri ikilinganishwa na wasichana.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo hayo Unguja, visiwani Zanzibar jana, alisema wavulana waliopata sifuri kwenye matokeo hayo ni 609, sawa na asilimia 1.37, huku wasichana wakiwa ni 369, sawa na asilimia 1.16.

Alisema kwa ujumla ubora wa ufaulu katika mtihani huo unaonyesha kuwa, kati ya watahiniwa wa shule waliofanya mtihani huo, 72,866, sawa na asilimia 95.52 wamefaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu.

Katika ufaulu huo, wasichana waliofaulu kwa madaraja hayo ni 30,619, sawa na asilimia 95.92 na wavulana ni 42,247, sawa na asilimia 95.23.

Alisema mwaka huu ufaulu umepanda kwa asilimia 1.52 ikilinganishwa na mwaka jana, ambako ulikuwa ni 96.06.

Alisema kwa matokeo ya jumla, watahiniwa 83,581, sawa na asilimia 97.58 wamefaulu, wasichana wakiwa 34,358, sawa na asilimia 98.26 na wavulana ni 49,223, sawa na asilimia 97.12.

“Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 75,305, sawa na asilimia 98.72, wasichana wakiwa 31.551, sawa na asilimia 98.84 na wavulana 43.754 sawa na asilimia 98.63 na kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 8,276, sawa na asilimia 88.35,” alisema.

Watahiniwa wa mtihani

Dk. Msonde alisema watahiniwa waliokuwa wameandikishwa kufanya mtihani walikuwa ni  87,571, wa shule wakiwa 77,155 na wa kujitegemea 10,416.

Alisema kati ya watahiniwa hao, wasichana walikuwa  35,380, sawa na asilimia 40.40 na wavulana 52,191 sawa na asilimia 59.60.

“Kati ya watahiniwa 87,571 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita Mei, 2018, watahiniwa 86,105, sawa na asilimia 98.33 walifanya mtihani na watahiniwa 1,466, sawa na asilimia 1.67 hawakufanya,” alisema Dk. Msonde.

Alisema watahiniwa wa shule waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 77,155, kati yao watahiniwa 76,734, sawa na asilimia 99.45 walifanya, wavulana wakiwa  44,757 sawa na asilimia 99.33 na wasichana 31,977 sawa na asilimia 99.62.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dk. Msonde alisema kati ya watahiniwa 10,416 waliosajiliwa, watahiniwa 9,371, sawa na asilimia 89.97 walifanya mtihani na ambao hawakufanya ni 1,045, sawa na asilimia 10.03.

Ufaulu kimasomo

Dk. Msonde alisema takwimu zinaonyesha kupanda kidogo kwa ufaulu wa masomo ya General Studies, Kiswahili, Physics, Chemistry, Biology, Basic Applied Mathematics, Advanced Mathematics, Commerce na Accountancy, ikilinganishwa na mwaka jana, huku masomo ya Historia, Jiografia, English Language, Agriculture Science na Economy ufaulu wake umeshuka kidogo.

Shule 10 bora

Dk. Msonde alizitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni Kibaha (Pwani), Kisimiri (Arusha), Kimebos (Kagera), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Ahmes (Pwani), St. Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Marian Girls (Pwani) na Feza Girls (Dar).

Shule za mwisho 

Inaendelea……………… Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Nimefurahia sana report yako! Kati ya magazeti yoote niliyopitia, hapa nimepata picha kubwa zaidi ya matokeo haya. Wengine wengi wametoa ripoti ya kishabiki, isiyoangalia mambo ya msingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles