31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AFICHUA MADUDU TIKETI ZA NDEGE ATCL

Na BENJAMIN MASESE – MWANZA


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele, amekutana na madudu mkoani Mwanza ambapo amesema licha ya bei elekezi za tiketi za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwa Sh 190,000, baadhi ya mawakala wanaziuza kwa Sh 400,000 hadi 450,000.

Kutokana na hali hiyo, Kamwele, wakati akizungumza na waandishi wa habari na wakuu wa idara zilizo chini ya wizara yake mkoani Mwanza, alisema: “Nimekutana na bomu la maajabu hapa Mwanza.”

Alisema licha ya mambo makubwa ya maendeleo kufanyika, bado baadhi ya maeneo yanatia shaka na kuna dalili za uhujumu uchumi hususani ndani ya ATCL na reli.

Akieleza hali ya ATCL, alisema haridhishwi na ukataji tiketi ambapo mawakala wanaotumiwa hawana ofisi maalumu, badala yake wanatumia vibanda huku bei elekezi ya chini kabisa kwa ndege za shirika hilo ni Sh 190,000 lakini wao huongeza na kufikia Sh 400,000 mpaka 450,000.

“Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani ilikuta shirika hili lipo hoi tena ni kama lilikuwa limekufa, lakini leo hii limefufuliwa na kuwa na ndege zake ambapo juzi tumeshuhudia tukipokea ndege kubwa ya Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 260, pia tunazo ndege za bombardier tatu.

“Ile ndege kubwa inatua viwanja vinne tu hapa Tanzania kikiwamo cha Mwanza,  ingawa kuna mambo ya kurekebisha haraka kabla ya kutua hapa Julai 29, lakini niseme wazi nimekutana na maajabu katika ukataji wa tiketi, yaani ATCL haina dirisha maalumu la kukata tiketi zake badala yake wanatumia mawakala.

“Mawakala wale hawana ofisi, wana vibanda tu, haiwezekani bei ya tiketi ya chini kabisa inakatwa zaidi ya Sh 400,000 wakati sisi tulielekeza iwe Sh 190,000, vile vile mawakla wale inaelezwa wana mikataba ya ajira na kampuni nyingine, kwa hiyo hapo kuna hali ya kuhujumu ndege zetu na shirika likafa tena,” alisema.

Waziri Kamwele aliwataka viongozi wanaohusika kumpa maelezo ya kina juu ya bei hizo kabla ya kuchukuwa hatua zaidi huku akitaka kufanyika kwa uboreshaji wa mfumo wa uthibiti wa ukataji tiketi.

Inaendelea……………….. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. maoni yangu kwa waziri,kama mawakala hao wepata vibali kutoka kwa serokali,kwanini wasifutiwe vibali hivyo? Bado mnawalealea kwahali hiyo kunakitu kinaendele weka wazi mheshimiwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles