28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAUZA NYAMA WAOMBA KIBALI CHA KUUZA NJE YA NCHI

Na JANETH MUSHI-ARUSHA


SERIKALI imeombwa kuwapatia wafanyabiashara wa nyama kibali cha kusafirisha ngozi  nje ya nchi ili kuweza kunufaika kiuchumi na kuliingizia Taifa mapato  zaidi.

Ombi hilo lilitolewa juzi na Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyabiashara wa Nyama jijini Arusha, Alex Lasiki, alipokuwa akizungumza katika hafla ya chama hicho kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Alisema Serikali imeruhusu kuuzwa mifugo nje ya nchi ambapo wakati mwingine wanalazimika kuuza mifugo hiyo bei ya chini, huku wanunuzi kutoka nchi jirani ya Kenya wakinufaika zaidi kutokana na kupata malighafi zaidi ikiwemo ngozi na pembe.

“Tunaiomba Serikali ituruhusu kusafirisha ngozi na malighafi nyingine zinazotokana na mifugo kwani itatusaidia kukuza mitaji yetu kama wafanyabiashara, lakini pia italiongezea Taifa kipato,” alisema.

Mwenyekiti huyo alitaja changamoto kubwa inayowakabili kuwa ni pamoja na kuwepo kwa  wimbi kubwa la mabucha feki yasiyokidhi viwango na  wengi wao kutokuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo na kuiomba Serikali kufanya msako wa kuwabaini watu hao wanaokiuka masharti ya biashara hiyo.

Naye  Diwani wa Kata ya Olorieni, Zakaria Mollel (Chadema) ambaye pia ni mfanyabiashara wa nyama, alisema kumekuwapo na urasimu mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara wanaosafirisha ng’ombe hao kwenda nchi jirani ya Kenya kutokana na wao kutolipa kodi na hivyo kuiingizia hasara Serikali.

Kutokana na changamoto hiyo, Mollel alisema ni vizuri Serikali ikaweka mnada katika mpaka wa Tanzania na Kenya wa  Namanga ili kuliingizia mapato Taifa na kuhakikisha wale wote wanaosafirisha mifugo kuwa na leseni na hatimaye kuweza kulipa kodi.

Kwa upande wake Ofisa Biashara kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha, Godfrey Edward, alikitaka chama hicho kuanzisha uongozi wao katika kila kata ili waweze kudhibiti uanzishwaji holela wa mabucha yasiyozingatia afya ya walaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles