24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAKAMU RAIS AFRIKA KUSINI AKIRI KUWA NA ‘MCHEPUKO’

PRETORIA, AFRIKA KUSINI


MAKAMU wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amekiri kuwa ana mpenzi nje ya ndoa, lakini amekana ripoti kuwa ana wapenzi wengi.

Ramaphosa alisema anaamini rasilimali za Serikali zinatumika kumchafulia jina ili kumzuia kuwania uongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC).

Chama hicho kinatarajia kuendesha uchaguzi miezi miwili ijayo, wakati Rais Jacob Zuma atakapong’atuka kutoka wadhifa huo.

Wachambuzi wa mambo nchini hapa wanasema inaonekana kuwa barua pepe za Ramaphosa, zilidukuliwa ili kuthibitisha uhusiano wa kimapenzi kati yake na daktari mmoja.

Lakini juzi Ramaphosa alijaribu na kushindwa kuzuia gazeti moja kuchapisha taarifa hizo.

Barua pepe hizo zilisema Ramaphosa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa wanawake kadhaa wenye umri mdogo.

Ramaphosa ni mume wa Tshepo Motsepe, ambaye ni dada wa bilionea wa hapa, Patrice Motsepe.

Wiki mbili zilizopita, Kiongozi wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Kiuchumi (EFF), Julius Malema, alifichua kwamba anafahamu kuwapo kampeni zinazomlenga Ramaphosa, ikiwamo tuhuma za kupiga wanawake.

Lakini mke wake wa zamani, Hope Ramaphosa, alijitokeza mara moja kumtetea.

“Cyril atachagua kujadiliana au kufanya vitu kwa busara kuliko kupiga mtu. Nilikuwa rafiki yake wa kike na baadaye mkewe kwa kipindi kirefu. Namfahamu Cyril vilivyo, hana tabia hiyo ya kupiga wanawake. Anaguswa na kujali mno na masuala ya haki za wanawake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles