28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI YASIFIA JARIBIO JINGINE LA NYUKLIA

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI


KOREA Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia jaribio bomu la nyuklia, ambalo linaweza kuwekwa kwenye kombora la masafa marefu.

Taifa hilo la kikomunisti lilisema jaribio hilo la sita la bomu la nyuklia, lilifanikiwa saa kadhaa baada ya mitetemeko mitatu kutambuliwa.

Ilidai kulifanyia jaribio bomu la haidrojeni, ambalo lina nguvu zaidi kuliko bomu la nyuklia.

Wadadisi wanasema kuna ishara kuwa uwezo wa nyuklia wa Korea Kaskazini unazidi kukua.

Watabiri wa hali ya hewa mapema walitambua uwapo wa tetemeko dogo la ardhi, eneo ambalo Korea Kaskazini ilikuwa ikifanyia majaribio ya nyuklia.

Tetemeko hilo lilitokea saa kadhaa baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kupigwa picha akiwa na kile ambacho vyombo vya habari vilisema kuwa aina mpya ya bomu la hydrogen.

Vyombo vya habari vilisema kuwa kifaa hicho kinaweza kutundikwa kwenye kombora la masafa marefu.

Muda mfupi baadaye Rais wa Korea Kaskazini, Moon Jae-in aliitisha mkutano wa dharura wa baraza za lake la usalama wa taifa.

Ripoti za awali kutoka kwa Idara ya Hali ya Hewa ya Marekani zilitaja tetemeko hilo kuwa la ukubwa wa kipimo cha 5.6 Richter, lakini baadaye likasema kuwa ukubwa huo ni 6.3 Richter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles