23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MERKEL KUICHUKULIA HATUA UTURUKI

BERLIN, UJERMANI


KANSELA  Angela Merkel, ametoa  wito wa kutafakari upya mtazamo  wa Serikali  ya Ujerumani  kwa Uturuki baada ya taifa hilo kuwakamata raia wao wawili zaidi.

Uhusiano kati  ya  nchi  hizo  mbili umelegelega tangu jaribio lililoshindwa  la mapinduzi mwaka 2016.

“Hakuna msingi wa  kisheria wa kukamatwa  kwao,” alisema Merkel akielezea  kuhusu Wajerumani hao waliokamatwa Alhamisi iliyopita nchini  Uturuki.

Kukamatwa kwao kunafikisha idadi  ya  raia  wa Ujerumani  waliokamatwa  nchini  humo  kwa sababu  za  kisiasa  kuwa 12.

“Hii  ndiyo  sababu  tunahitaji kuchukua  hatua  muhimu  hapa,” alisema na  kuongeza  kwamba  Serikali yake inapaswa kutafakari  upya uhusiano  wake na  Uturuki.

Merkel  alisema  Ujerumani  tayari imeendeleza  kwa  kiasi kikubwa  uhusiano wake  na  Uturuki, lakini  hatua   hii  mpya  ina maana huenda  ni  muhimu  kutafakari  upya zaidi.

“Madai yetu kwa  Uturuki yako  wazi  kabisa,” alisema msemaji  wa  Serikali ya  Ujerumani,  Steffen Seibert.

“Tunatarajia Uturuki itawaachia  huru  raia  wa  Ujerumani  ambao  wamekamatwa  kwa misingi isiyokuwa ya  kisheria.”

Mahusiano baina  ya  washirika  hao  wa  Jumuiya ya Kujihami ya NATO yamevurugika tangu  Serikali  ya  Ujerumani  ilipoikosoa  Uturuki  kuhusu ukandamizaji  uliofuatia  jaribio la  mwaka  jana  la mapinduzi lililoshindwa.

Mwisho

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles