31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Wauza maji Dar watakiwa kujisajili Dawasa

Tunu Nassor 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), imewataka wauzaji wa majisafi kwa kutumia visima wafike katika ofisi za mamlaka hiyo kuanzia Oktoba 28 ili kuwatambua na kuwasajili.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 23, Mamlaka hiyo, ikiwataka wamiliki hao waliopo ndani ya Dar es Salaam kufika na taarifa za wateja wanaowahudumia, vyeti vya ubora wa maji na taarifa za visima ambapo watoa huduma wametakiwa kufika ofisi za Dawasa Gerezani.

Dawasa imesema lengo ni kutambua watoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za majisafi kwa wananchi.

“Lengo kutimiza matakwa ya kisheria inayoitaka Dawasa kuwatambua na kuwasajili kwa kuwapatia cheti cha utoaji huduma za maji safi kwa watoa huduma za maji ,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema Dawasa ndio chombo kilichorasimishwa kisheria kusimamia huduma za usambazaji maji safi ndani ya eneo lake la huduma ambalo ni jijji la Dar es Salaam, miji ya Mlandizi, Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga Mkoa wa Pwani.

“Utoaji vyeti utafanyika kwa muda wa mwezi mmoja baada ya tangazo hili na muda wa usajili ukipita mtoa huduma yoyote asiye na cheti cha kutoa huduma hataruhusiwa kuuza maji,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa hakutakuwa na tozo zozote katika utoaji wa vyeti hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles