Watu 19 wauawa kituo cha walemavu Japan

knife1_article_main_image

Toyko: Japan

KIJANA mmoja nchini Japan amewashambulia kwa kisu na kuwaua watu 19 na kujeruhi wengine  26 kwenye kituo cha walemavu cha Sagamihara nje kidogo mwa mji mkuu,  Tokyo.

Satoshi Uematsu (26), alivamia kituo wakati watu wakiwa wamelala na kuwashambulia kwa kisu.

Uematsu aliwasiri katika kituo cha Tsukui Yamayuri En  saa 8.10 alfajiri na polisi walifika eneo la tukio baada ya dakika 20.

Wanawake 9 na wanaume 10 wenye umri  kati ya miaka 18 na 70 ndiyo waliouawa  katika tukio hilo.

Taarifa kutoka  Japan zinasema mtuhumiwa huyo alikuwa akifanya kazi katika kituo hicho cha Tsukui Yamayuri En  kabla ya kufukuzwa kazi.

Muuaji huyo alijisalimisha katika  kituo cha polisi na kukiri kutekeleza mauaji hayo ya kutisha na akawekwa chini ya ulinzi.

Polisi wanasema mtuhumiwa huyo alikuwa amemwandikia barua spika wa bunge   Februari mwaka huu akitishia kuwaua walemavu.

Baada ya tukio hilo alipelekwa  hospitalini kutibiwa na baadaye akaachiwa.

Gazeti la moja   Japan,  Asahi Shimbun, limeripoti kuwa kijana huyo aliwaambia polisi kuwa anataka kuwaondoa walemavu wote  duniani.

Inasemakana mauaji kama hayo  hayajawahi kutokea nchini  humo tangu Vita ya Pili ya Dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here