29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Koffi Olomide akamatwa DR Congo

Koffi Olomide
Koffi Olomide

KINSHASA, DR CONGO

MWANAMUZIKI mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide, amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa nchini humo kutokana na tukio la kumpiga teke mwanamuziki wake walipowasili nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliopita.

Olomide alifukuzwa nchini Kenya kutokana na kuenea kwa video ambayo ilimuonesha msanii huyo akiwa anampiga msanii wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Alipanga kutumbuiza mashabiki wake kwenye ukumbi wa Bomas nchini Kenya Jumamosi, lakini tamasha hilo liliahirishwa na msanii huyo kurudishwa nchini kwake ambapo jana alikamatwa na polisi.

Hata hivyo, msanii huyo alitakiwa kwenda kutumbuiza mashabiki wake nchini Zambia, lakini kutokana na tukio hilo Shirika la Kilimo na Biashara la nchini Zambia, limefutilia mbali tamasha hilo ambalo lilitakiwa kufanyika Agosti mosi mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Jumapili ya wiki iliopita, msanii huyo aliomba radhi mashabiki wake na hasa ‘wanawake na watoto’.

“Najutia sana yaliyotokea, ilikuwa ni kipindi kifupi cha wendawazimu wangu, lakini ninaomba radhi kutokana na tukio hilo,” aliandika Koffi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles