24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wahimizwa kuchanja chanjo ya corona

Na Shomari Binda, Musoma

Watanzania wamehimizwa kuendelea kujitokeza kuchanja chanjo ya Corona kwa kujilinda kwa kuwa imethibitishwa kuwa ni salama.

Hayo yameelezwa jana na mjumbe wa Baraza Kuu la Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mara, Rhobi Samwel, alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya.

Amesema afya ni jambo la msingi na kwa kuwa chanjo imethibitishwa kuwa ni salama hivyo ni muhimu kila mmoja kuchanja na kujilinda na maambukuzi.

Rhobi amesema mwanamke kwenye familia ndio nguzo ya malezi na anapokuwa na afya njema anaisimamia vyema familia na kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Amesema sio wanawake pekee bali kila mmoja anapaswa kuona umuhimu wa kuchanja chanjo hiyo ya corona ili kujikunga na janga hilo.

“Tuko hapa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya lakini ni muhimu kuzungumzia suala la afya kwa kipindi tulicho nacho.

“Rais wetu Mama Samia ametuambia chanjo ni salama ni muhimu tukachanje ili tuendelee kuwa salama na kufanya kazi ili kuinua uchumi,” amesema Rhobi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara, Wegesa Hassan, wakati wa kutoa tamko la kumpongeza Rais Samia, amesema yapo mengi ambayo anaendelea kuyafanya ambayo yanastahili pongezi.

Amesema kwa mkoa wa Mara sasa inatolewa huduma ya kusafisha figo kwenye hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuwapa unafuu wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles