24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC aahidi neema kwa wananchi, Viongozi Ilemela

Na Sheila Katikula, Mwanza

MKUU wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Hassan Masala amesema atashirikiana na viongozi wa idara mbalimbali pamoja na wananchi ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili  kwenye maeneo yao.

Masala amesema hayo katika mkitano wa hadhara kwenye kata ya Buswelu wilayani Ilemela jijini hapa na kusisitiza kila kiongozi anawajibu wa kusimama kwenye nafasi yake na kutimiza  majukumu kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na serikali.

Alisema  lengo la ziara hiyo ya kuzingikia kata 19 za wilaya hiyo ni  kutembelea miradi iliyopo na kuzungumza na wananchi ili kuweza  kutambua changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao.

“Nimesikia mkizungumza kwa uchungu  kuwa mnakabiliwa na changamoto ya umeme,maji kwenye maeneo yenu naomba tushirikiane kwa pamoja kwa sababu nyinyi ni sehemu ya kutatua nisingependa kusikia nikirudi tena baada ya miezi mitatu  yanazungumziwa  masuala haya.

Aidha amewataka viongozi kuacha kukaa ofisini na badala yake kutoka nje na kuzungumza na wananchi  kwa kufuata sheria na taratibu  zilizowekwa kwani dhamira ya serikali ni kuhakikisha wanatekeleza  ahadi zote kwa wananchi.

Meneja wa shirika la umeme Tanesco Nyakato, Mhandisi Edward Kweka amesema jitihada zinaendelea  kufanyika kuhakikisha  wananchi waliopo kwenye kata hiyo wanapata huduma hiyo  kwa muda uliopangwa  ili kuondoa kero  ya umeme kwa wananchi ambayo wamekuwa  wakiipigia kelele kwa muda mrefu.

Aidha  Meneja wa kanda Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Mkoani Mwanza Kanda ya Nyakato na Kisesa, Mhandisi Josephat Ilunde amesema ifikapo  Novemba 30 mwaka huu  mradi wa maji uliopo kata ya Buswelu utakamilika na kupunguza  changamoto  hiyo kwa wananchi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles